Bayport yatoa Milioni 15 kusaidia watoto 300 Muhimbili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma, imejitolea Shilingi milioni 15 kusaidia gharama ya matibabu ya watoto 300 wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Msaada huo umeenda sanjari na maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyoadhimishwa jana Machi 8, ambapo msaada huo umedhuhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi pamoja na baadhi ya watumishi wa Bayport Financial Services Ltd.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Utawala wa Bayport Financial Services, Suzan Kolimba, alisema taasisi yao imeguswa na changamoto wanazopitia watoto hali iliyowafanya wajitolee msaada huo.

Alisema tangu mwaka 2006 walipoingia kwenye sekta ya mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma, wamekuwa wakijitolea misaada mbalimbali kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Watanzana waliochagua kuhudumiwa na Bayport.

“Bayport ndio taasisi ya kwanza iliyoanzisha huduma ya mikopo kwa njia ya kidijitali mwaka 2019 bila kujaza karatasi yoyote, ambapo ili mteja apate huduma yao atapiga simu ya bure 0800782700 na kupata mkopo wa haraka wa haraka.

“Hali hii inatufanya tuone thamani ya Watanzania wanaoendelea kuichagua Bayport kupata huduma za mikopo ya fedha, ndio maana tunaona haja ya kujitolea msaada wa matibabu kwa watoto hawa 300 hapa Muhimbili,” Alisema Suzan.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Janabi, aliwashukuru Bayport kwa kitendo cha kusaidia gharama za matibabu kwa watoto hao na kuwataka waendelee kujitolea kwa jamii kwa manufaa ya Taifa.

“Huu ni msaada mkubwa kwa watoto hawa hivyo Bayport muendelee kujitolea kwenye jamii yetu kwa sababu ni jambo zuri mno mmefanya.

“Sasa wazazi na walezi wa watoto hawa angalau watakuwa wamepungukiwa na gharama za matibabu kwa sababu nyie mmejitokeza kuwasaidia,” Alisema Janabi.

Huduma za mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma kupitia Bayport zimerahishwa kutokana na mfumo wao wa kukopa kidijitaji ambapo mteja anapiga simu ya bure 0800782700 au kuingia mtandaoni www.kopabayport.co.tz kupata huduma hiyo bila kujaza makaratasi yoyote.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Ltd, Suzan Kolimba wa tatu kutoka kushoto mbele, akiwa na baadhi ya watumishi wa taasisi yao walipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kutoa msaada wa matibabu kwa watoto 300 kwenye hospitali hiyo wenye thamani ya Sh Milioni 15. Picha na Mpigapicha wetu.






No comments