UZINDUZI WA LISHE APP KUHUSU KUJENGA UELEWA WA LISHE BORA -MACHI 6
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
TAASISI ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC) kwa kushirikiana na Shirika
la Chakula Duniani (WFP) wametengeza ‘Lishe App’ kwa lengo la kuongeza kasi ya
kuwajengea uelewa wananchi kuhusu umuhimu wa lishe bora pamoja na
kuchochea mabadiliko chanya ya tabia za ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha kwa WAVIU kwani kundi hilo mojawapo maalum
lenye mahitaji ya kilishe.
Akizungumza leo Machi 6,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kuzinduliwa kwa Lishe
App, Mgeni rasmi kwenye tukio hilo ambaye ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumain Nagu amesema anaamini Lishe App itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu na ujuzi wa namna ya kuandaa mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo husika.
Aidha amesema hiyo ni fursa mojawapo ambayo itasaidia kuchangia kufikia malengo ya Wizara ya Afya kukinga na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza, hususan magonjwa yatokanayo na lishe duni kwani takwimu
zinaonesha zaidi ya watu milioni nne wanatumia simu janja zenye uwezo wa
kupata taarifa sahihi za lishe kupitia app hii.
“Ili kufanikisha malengo ya Serikali na Wizara ya Afya, natoa maagizo yafuatayo
kwa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kuongeza jumbe za lishe kwa makundi
mengine yakiwemo ya watu wenye magonjwa ya sukari na saratani, watoto
wadogo na wachanga, vijana balehe na wajawazito na wanawake wanaonyonyesha.
“Lengo ni kuongeza chachu ya mabadiliko chanya katika ulaji unaofaa na mitindo bora wa maisha kwa watu wote. Kubuni njia za kuwafikia wanaume ili kuleta uelewa wa pamoja katika familia kwa lengo la kukinga badala ya kutibu.Kupokea mrejesho toka kwa watumiaji/walengwa na kuendelea kufanya maboresho.
“Pia kuweka huduma itakayomsaidia mtumiaji kufanya tathimini ya kiasi ya
chakula alichokula na mpangilio wa mlo kama unatimiza vigezo vinavyotakiwa
kulingana na shughuli anayoifanya. Kufanya jitihada za kuitangaza App hii kwa jamii ya kitanzania ili ifahamike na kutumiwa na watu wengi zaidi.Pia hakikisheni App hii inakuwa endelevu kwa kuweza kujiendesha yenyewe,”amesema Profresa Nagu.
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa namna ya pekee wote walioshiriki katika
utengenezaji wa Lishe App wakiwemo wataalam kutoka Taasisi ya Chakula na
Lishe Tanzania.“Nitoe mwito kwa wananchi wote kutumia Lishe app hii katika kutafuta na kupata taarifa sahihi za lishe.
“Kwani sasa hivi kumekuwa na wimbi kubwa la ongezeko la taarifa potofu kuhusu
masuala ya chakula na lishe hususan katika mitandao ya kijamii.

Pia niviombe vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu ya afya na lishe pamoja na kuitangaza lishe app pamoja na kuhamasisha jamii kuitumia ili kuleta mabadiliko chanya ya tabia katika suala la afya na lishe.
Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa hali ya lishe ni mojawapo ya viashiria
muhimu ambavyo Taifa linavitumia kupima maendeleo ya mtu mmoja mmoja, jamii
inayomzunguka na Taifa kwa ujumla.
Hivyo lina umuihimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii Kitaifa na kutokana na hilo Serikali imebainisha masuala ya lishe katika Sera ya Afya ya mwaka 2007; Ilani ya Chama Tawala (CCM) 2020-2025; Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo 2021/22 – 2025/26 na; Mpango Jumuishi wa Pili wa
aifa kuhusu masuala ya Lishe 2021/22 – 2025/26.
Pamoja na mambo mengine amesema utafiti wa mwaka 2016 uliofanyika Dar es salaam ulibainisha asilimia 16 ya WAVIU wana uzito uliozidi na asilimia nane wana kiribatumbo.

“Sote tunafahamu kuwa Taifa letu, chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya
sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan linatoa kipaumbele katika masuala ya afya na lishe.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC)Dk.Germana Leyna katika kutekeleza majukumu yao wanajitahidi kuhusisha
makundi mbalimbali ili kuhakikisha jumuiya yote ya watanzania wanapata taarifa sahihi ya masuala ya ulaji .
Aidha amesema mwaka 2020 walifanya tafiti katika mikoa ya Geita na Singida kuangalia hali za lishe na uelewa wa huduma za afya na sababu ya kwenda huko ni kutokana na toka miaka 2000 mwanzoni walikuwa wakitoa elimu ya namna gani ya kufanya unasihi kwa watu ambao wanaishi na virusi
vya Ukimwi.
“Tumekuwa tukitoa elimu kwa watoa huduma za afya lakini tulitaka kufahamu
wale wahusika wenyewe ambao ni watu wenye maambukizi ya UKIMWI wana
ufahamu na tulifanya utafiti huo tuliweza kufanya tu mazungumzo ya ana kwa ana na watu takribani 20 na kati yao 18 walikuwa hawana taarifa kamili.

“Hali hiyo kwetu ilikuwa kiashiria kwamba elimu hii haijafika watu , tuliona bado elimu inahitajika kwa hiyo lazima tutafute njia ambayo itakuwa rahisi kufikia watu wengi zaidi katika kutoa elimu, ndipo tukaja na wazo la kutumia App ya kiganjaji na
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumain Nagu(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Idara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Wawakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP), Ofisi ya Mganga Mkuu mkoa wa
Dar es Salaam , Mwakilishi wa Mtandao wa Wanawake wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Baraza la Watu Wanaoishi na VVU baada ya kuzinduliwa rasmi ‘Lishe App’
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumain Nagu(kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Obery Assery (katikati)Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP)Sarah Gordon –Gibson(kushoto) wakiwa
makini kupata maelekezo kutoka kwa mmoja ya watalaam waliotengeneza Lishe App kabla ya kuizundua rasmi.
Baadhi ya wawakilishi wa WFP pamoja na wadau wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Lishe App ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa ujumbe
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumain Nagu(aliyesimama) akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa Lishe App .Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za Taasisi ya Chakula na Lishe jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali kwenye picha wakati wa uzinduzi wa Lishe App uliofanyika leo Machi 6,2023 jijini Dar es Salaam(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE wa MICHUZI TV)
Post a Comment