Mhandisi Jafari ajitosa kupambana na Babu Tale
Awali, Mhandisi Jafari alikabidhiwa fomu na katibu wa CCM wilaya comrade Michael Bundala na kufanikiwa kuirudisha.
Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea wanaowania nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Mbunge aliyemaliza muda Hamis Taletale ( Babu Tale)
Mhandisi Jafari amesema ameguswa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuwaletea maendeleo kwa haraka kwa kushirikiana na viongozi wa chama jimboni humo pamoja na Serikali.
" Nikiwa kijana mwenye nguvu na kubobea katika mikakati ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi nimeona wakati umefika wa kuwa mtumishi wa watu wa jimbo hili,"
" Hivyo, naomba ridhaa ya chama changu na wananchi kunipokea kwa mikono miwili ili tujiletee maendeleo ya haraka,", amesema.
Post a Comment