DKT. EGBERT MKOKO: BLOGU ZISITUMIKE VIBAYA UCHAGUZI MKUU
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza katika mafunzo maalumu ya bloga yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ombi la Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN), Dkt. Mkoko alisema blogu zina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii, hivyo zinapaswa kutumika kwa uangalifu na weledi.
“Blog zina nguvu kubwa ya kusambaza taarifa kwa jamii, hivyo mnapaswa kuzitumia vizuri hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaingia kwenye uchaguzi mkuu,” alisema.
Alibainisha kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Mwongozo wa Uandishi wa Habari za Uchaguzi ili kuhakikisha taarifa zinazochapishwa zinachangia kudumisha amani na utulivu nchini.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, aliwakumbusha wanahabari kuepuka kuandika taarifa za uzushi na uchochezi ambazo zinaweza kusababisha taharuki. Alisisitiza umuhimu wa kutoa nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa na kuthibitisha ukweli wa taarifa kwa mamlaka husika kabla ya kuziweka hadharani.“Akili Bandia ikitumika vizuri inaongeza ufanisi wa mawasiliano, lakini ikitumiwa vibaya inaweza kuwa na madhara makubwa. Ni jukumu la watumiaji kuzingatia maadili na weledi,” alisisitiza.
Mafunzo hayo yamekusudia kuwajengea uwezo waendeshaji wa blogu kuhusu uandishi wa habari za uchaguzi, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na teknolojia mpya ili kuchangia uchaguzi wenye amani na maadili.




Post a Comment