Sangu Atoa Siku 3 TARURA Kuanza Ujenzi Daraja la Ilambo

Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, ametoa siku tatu kwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha Mkandarasi anaanza mara moja ujenzi wa Daraja la Ilambo kuanzia Desemba 27, 2025.


Mhe. Sangu amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tayari imetoa zaidi ya shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja matatu, ambayo yanapaswa kukamilika ndani ya miezi sita.

Ametoa kauli hiyo leo, Desemba 24, 2025, katika Kata ya Kwela mkoani Rukwa, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madaraja, akisisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutaondoa adha kwa wananchi wanaotegemea miundombinu hiyo kwa shughuli zao za kila siku



 

No comments