KATIBU MKUU CCM AAGIZA MTENDAJI MKUU TARURA AANDIKIWE BARUA HARAKA ILI BARABARA YA MBULU-HAIDOM ITENGENEZWE
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Mbulu
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Daniel Chongolo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) Mkoa wa Manyara kuandika barua haraka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo ili ipatikane fedha kwa ajili ya kujenga barabara ya Mbulu ambayo kwa sasa ni mbovu.
Akizungumza leo Machi 6,2023 wilayani Mbulu mkoani Manyara ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika Mkoa huo, Chongolo amesema barua hiyo kwa Mtandaji Mkuu iandikwe leo na atazungumza na Mtendaji Mkuu atafute fedha kokote ili barabara hiyo irekebishwe.
“Sikiliza maelekezo yangu andika barua le oleo kwa Mtendaji Mkuu , mwambie Meneja wako aandike leo kisha nitumie mimi na umtumie na yeye, na nitazungumza naye , hatuwezi kimya wakati barabara inahitaji udharura kwani imeshaharibika sana .Madaraja yapo lakini maeneo mengine hali sio nzuri, tunataka barabara irekebishwe na mimi kazi yangu rahisi tu ,wewe usitekeleze mimi baadae nitanong’ona na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Kama wanajipenda warekebishe hiyo barabara, kama Mbulu mkandarasi ameanza kutengeneza barabara hatuwezi kuacha huku kukabaki kuliko, ni sawa na kuvaa tai halafu umevaa kamptula. Yaani huku kichwani kujengwa kule miguuni kumeachwa, sio sawa.Hivyo leo andika hiyo barua.Tunataka fedha ya dharura ije na najua itapatikana.
“Na kama fedha haijapatikana basi hata mimi sipaswi kuwa Katibu Mkuu, maana siwezi kumwakilisha Mwenyekiti wa Chama chetu halafu mambo yako hayaendi, lazima ujue unayemwakilisha ni mzito na uwakilishi lazima uwe kwa uzito wake.”
Wakati anazungumzia barabara hiyo Chongolo amesema Mbunge wa Jimbo la Mbulu amezungumzia barabara mbili ikiwemo inayotokea Mbulu Mjini kuja Haidom mpaka Singida na Mkandarasi ameshapewa kilometa 25 , lakini fedha bado haijatoka ,hivyo yeye ndio bosi wa mawaziri wote na ndio anayewasimamia kwani wamepewa jukumu la kutekeleza Ilani.
“Na mimi ndio mwenye Ilani ,ndio mtendaji Mkuu wa Ilani hiyo, siko tayari kuona mambo yanachelewa kuleta matokeo tuliyoahidi kwa wananchi kama wameweka kilometa 25 na hawajatoa fedha wamejitengenezea nongwa naenda kuwaagiza waongeze kilometa 25 nyingine ziwe kilometa 50.
“Hatuwezi kuwa tunawaambia wananchi tunaleta tunaleta wakati wanataka waone tumefika tumefika tumefika na mimi niwaambie leo asubuhi nimezungumza kirefu sana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye nimemwambia leo nakuja Mbulu.
“Akaniambia (Rais)ukienda wapelekee salamu zangu za dhati, ninyi mshaanza kuchochea kidogo huyu Waziri wa Ujenzi hajanza kushughulika na barabara ya Mbulu mkapa Haydom kwenda Singida na yeye akaniambia nenda kaone upande wa Mbulu nini kinandelea halafu jioni tutazungumza, hivyo tutamaliza hadithi ya hii barabara ndio kazi ya Serakali .
“Mimi kazi yangu ni ndogo tu kumwambia Rais Waziri wako hajapeleka fedha , kazi hiyo naiweza na niko timamu na mbunge nikuhakikishie wala huna haja ya kwenda kuruka sarakasi tena bungeni , ni kutamka na jambo kutokea hatuwezi kuwa na watu tuliowapa jukumu la kutekeleza mipango tuliyopanga na kuahidi na wao wakaa kienyeji, “amesema Chongolo.
Hivyo amesema wanataka wakae sawa sawa wajue wanawajibu wa kufanya na kubadilisha matokeo kuwa tija kwa wananchi huku akifafanua amefika Mbulu na hiyo barabara kwa kweli hajafurahishwa nayo kwani ni mbovu kabisa na haifanani na shughuli za maendeleo wanazofanya.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo leo ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Gunyoda, Mbulu ambalo mpaka kukamilika litagharimu shilingi 839,760,000.

“Imeniuma na niwaambie wasituletee hadithi ya bajeti, bajeti ni mdudu gan? Tunataka barabara itengenezwe na ipitike vizuri wakati wote bila matatizo, niwahakikishie leo nina ziara na sijaja kupiga porojo nimekuja kusikiliza shida za wananchi nikahangaike nazo.
“Chama tawala ni kikubwa na nimeichukua hiyo barabara naenda nayo, muwe na imani barabara hiyo itafanyiwa kazi.

Post a Comment